Wabaptist: Mashujaa wa Uhuru wa Kidini
“… mliitwa mate uhuru: lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”
Wagalatia 5:13
Mchungaji mashuhuri wa Baptist George W. Truett (1867-1944) kwenye mahubiri yake yenye kisa cha Wabaptist na uhuru wa dini alimnukuu Mwana historia wa Kimarekani George Bancroft alichokisema, “Uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa maoni, lilikuwa taji la kwanza kwa Wabaptist.”
Truett pia alimnukuu Mwanafalsafa wa Kiingereza John Locke’s alichokisema, “Wabaptist walikuwa wa kwanza kugundua uhuru kamili, wa haki na wa ukweli kabisa, wenye usawa na uhuru ambao ndani yake hakuna upendeleo.”
Ugumu wa kuwa na Uhuru wa Kidini
Ni dhahiri, Wabaptist ni miongoni mwa viongozi ambao walipata ugumu wa kuwa na uhuru wa kidini, lakini kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu sana. Ni kweli, uhuru wa dini umekuwa, na bado unakuwa, kwa mara chache sana na ugumu wake. Wakati wa vuguvugu la kudai Ukristo, viongozi wa serikali waliwatesa sana Wakristo. Tangu zama za kati na vuguvugu la kudai mabadiliko ya kidini, uhuru wa dini kwa uhalisia haukuwepo, kwa sababu makundi yote mawili ya Waroma na Makanisa ya kiprotestant walikuwa wakiomba msaada kwa serikali ili kupambana na wale waliokuwa hawakubaliani na mafundisho yao.
Huko Uingereza, Thomas Helwys (1556- 1616), alitambuliwa kama Mchungaji wa kwanza wa Baptist kwenye ardhi ya Uingereza, aliyethubutu kupinga kauli ya Mfalme juu ya kujingilia masuala ya kidini. Helwys w aliandika kijitabu mnamo mwaka 1612 chenya kichwa The Mystery of Iniquity (Siri ya Maovu) na akatuma nakala ya hicho kitabu kwa Mfalme James 1 na maelezo yake binafsi akisema, “Mfalme ni mtu wa kawaida na wala sio Mungu, hivyo basi hana mamlaka juu ya roho za watu kiasi cha kuwapangia amri na kuwapa maagizo ya namna ya kufanya huduma za kiroho dhidi yao.”
Kwa Helwys’ kitendo chake cha ushujaa na kuendelea kusimamia mafundisho ya Kibaptist juu ya uhuru wa dini, Mfalme James alimtupa gerezani Helwy’s na umauti ukamkuta huko…. Kwa sababu ya kudai uhuru wa kidini, sio tu kwa ajili ya Baptist lakini kwa ajili ya watu wote pia. Watu wengi walipata shida na hili. Kwa mfano, John Bunyan (1628- 1688), mwandishi wa kitabu cha Pilgrim’s Progress(Safari ya Mahujaji), aliteswa sana kwenye magereza ya Uingereza kwa sababu ya kuwa Mchungaji wa Baptist hakukubaliana na ukandamizwaji wa uhuru wa dini.
Huko Marekani, Roger Williams (1603-1683) aliteswa kwa sababu ma maoni yake juu ya uhuru wa kidini. Mnamo Janiuary 1636, alikimbilia huko Massachusetts na kuwa mkimbizi na rafiki yake wa Kihindi. Wakati wa kifuku, alianzisha rasmi ukoloni wa kisiwa cha Rhode na alisisitiza ukuru wa kutoa maoni kwa raia wote. Pia alisaidia kuanzishwa kwa kanisa la Kibaptist upande wa Magharibi.
Hata hivyo, uhuru wa dini ulifanyika kama bidhaa adimu kwenye Dunia Mpya. Wabaptist walianzisha jitihada za hapa na pale upande wa mashariki ili kuleta uhuru wa dini, Wabaptist hadharani walikuwa wakinyanyaswa, kufungwa jela na kushtakiwa na mamlaka za kiserikali na kupigwa na kudhauliwa na watu bila hata huruma kwa sababu ya kudai uhuru wa dini.
Hatimae , kupitia jitihada za viongozi kama vile Isaac Backus (1724-1806) huko Uingeleza na John Leland (1754-1841) huko Virginia, kama sauti ya Wabaptist, wakiungana na wengine, waliweza kusikilizwa. Kwa mfano , Leland ilisadikika alikutana na James Madison chini ya mti wa mwaloni kwenye kijiji cha Orange , VA, na aliomba dhamana ya Madison ili aweza kuongeza kipengele kwenye Katiba mpya kinatakachoelezea uhuru wa dini. Katiba ya Marekani, awaali ilikuwa na kasoro ya kukosa kipengele cha uhuru wa dini, na baadae kipengele hicho kikaongezewa chini ya uongozi wa Madison ili kutoa ruksa. Kwa mara ya kjwanza kihistoria, kwa taifa kutoa uhuru kamili wa kidini kwa raia wake.
Msingi wa Uhuru wa Kidini
Kwa nini Wabaptist waliamua kutoa gharama kubwa ili kuweza kuwa na uhuru wa kidini? Kwa nini hawakutaka kukubaliana na hali ilivyokuweko badala yake kutaka uhuru wa kidini, na sio kwa ajili yao tu bali kwa watu wote? Jibu linapatikana kutoka kwenye msingi wa mafundisho ya Kibaptist juu ya asili ya imani ya Kikristo.
Kujitoa kwa Wabaptist kwa ajili ya uhuru wa kidini vinahusiana moja kwa moja na ukweli mwingine wa Kiblia ambapo ni pamoja na mafundisho ya Baptist na desturi yao. Uhuru ni sehemu muhimu sana kwenye haya.
- Uhuru wa kumfuata Kristo.Biblia inasema Jesu akiwa Bwana wa watu wote ametoa wito wa kumfuata yeye (Mathayo 7:21-27; 16:24-25). Huu ufuasi, hata hivyo, unapaswa kuwa huru, na sio wa kulazimishwa. Zaidi ya hapo, watu wanapaswa kuwa huru kumfuata Kristo, sio kuzuiwa na mamlaka yeyote ya kiserikali au na Kanisa lolote. Wokovu katika Kristo ni kwa imani kwa njia ya kuipokea zawadi ya neema ya Mungu, Mwanae (Waefeso 2:8-10). Uhuru wa kutangaza, kusikia, na kuitikia kwa hii habari njema ambayo haipaswa kupuuzwa.
- Uhuru wa kuisoma na kuelezea Biblia. Biblia ndiyo yenye mamlaka juu ya imani na desturi. Wabaptist husisitiza kwamba kila aaminie Kristo kwa imani hufanyika kuwa kuhani muumini akiwa na uweza wa Kimungu kuielewa na kuitumia Biblia kwa msaada wa Roho Mtakatifuhe. Hakuna Kanisa wala viongozi serikalini wenye mamlaka ya kuzuia watu wasisome Biblia wala kuzuia kile ambacho Biblia hufundisha. Kila mmoja anapaswa kuwa huru kufanya hivyo bila kipingamizi cha aina yeyote ile.
- Uhuru wa Kubatizwa.Wabaptist husisitiza kuhudumia yule tu ambaye kwa hiari amemwamini Kristo kwa imani (ptists insist that baptism ought to be administered only to someone who voluntarily commits to faith in Christ (Warumi 6:3-5; Wakolosai 2:12). Ubatizo usilazimishwa kwa mtu yeyote, wala asiwepo wa kumzuia mtu asibatizwe.
- Uhuru wa kuchagua na kusaidia Kanisa. Bibllia hufundisha kwamba Kanisa ni ushirika wa hiari wa waumini waliobatizwa katika Kristo ambao kwa hiari kusaidia huduma (Matendo 2:47; 2 Wakorintho 9:7). Wabaptist , kwa hiyo, kwa nguvu zote hupinga Makanisa yanayomilikiwa kiserikali au hutumia fedha za kodi ili kuendesha Makanisa.
- Uhuru wa kuongoza Kanisa. Kwa Kristo na kwa njia ya Roho Mtakatifu, makuhani waumini wana uwezo mkubwa wa kujiongoza kwenye Kanisa linalojitegemea (Matendo 6:1-6; 13:1-3; 1 Wakorintho 5:1-13). Hivyo basi, wako huru kufanya hivyo kikubwa jitihada za kuwazuia kutoka kwa Kanisa au kutoka kwenye mamlaka ya Kiserikali kikubwa hali ya afya na usalama wa raia usiingiliwe.
- Uhuru wa kushuhudia na kuhudum. Wabaptist huamini kwamba makuhani waumini wanao wajibu wa kueneza injili na kuwahudumia wengine kupitia jina la Kristo. Hivyo Wabaptist hutoa wito kwamba watu wanapaswa kuwa huru kushuhudia na kuhudum bila kuingiliwa na mamlaka yeyote ya kibinadamu (Matendo 5:29-42).
Kuutumia Uhuru wa Kidini
Wabaptist wa zamani walilipa gharama kubwa sana ili kusaidia uwepo wa uhuru wa kidini kwa watu wote. Ni yepi ambayo Wabaptist wa sasa wanapaswa kufanya juu ya huu urithi wenye thamani?
- Kulinda uhuru wa kidinikujitoa kwa udhabiti ndio gharama ya uhuru, pamoja na uhuru wa kidini. Huchukua kizazi kimoja au viwili kupoteza kwa kukataa kile ambacho vizazi vingi vitafaidi kwa njia ya kujitoa.
- Kuendeleza jitihada za kuwa na uhuru wa kidini.Watu wengi ulimwenguni hawaishi vema mahali ambapo hamna uhuru wa kidini. Mateso na watu wa dini na mamlaka ya kiserikali bado kunaendelea.
- wajibika ipasavyo na uhuru wa kidini.Onyesha uwajibikaji kwa kuwa huru kuisoma Biblia, kuwa msaada kwa Kanisa, kwa kuwashuhudia wengiene, na kuishi maisha ya utaua sambamba na mafundisho ya Yesu.
- Kusimamia kutenganishwa baina ya Kanisa na Serikali. Uhuru thabiti wa kidini ni mambo mawili tofauti na taasis za kidini na mamlaka ya kiserikali. Wabaptist wameliweza hili na wanapaswa kuendelea na huo msimamo.
- Utumie uhuru kwa faida yaw engine. Paulo aliandika, “mliitwa mate uhuru: lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”(Wagalatia 5:13) Hivyo tunapaswa kutumia uhuru wetu, sio ubinafsi, lakini kwa njia ya kutoa huduma kwa wenye uhitaji duniani kote.
Hitimisho
Kwa hali ya juu na gharama kubwa Wabaptist walisaidia kupatikana kwa uhuru wa kidini kwa ajili watu wengi sana kwenye hiki kizazi. Sasa ni juu ya Wabaptist wa sasa kusaidia kuutunza huu uhuru kwa ajili ya vizazi vya baadae.
“Ni ngumu kuwaelezea Wabaptist bila kuelezea kujitoa kwao
kwenye hali ya kudai uhuru kamili wa kidini.”
William R. Estep
Kwa Nini Wabaptist?