Wabaptist : Kuishi Ipasavyo Injili
“… Na Bwana anataka nini kwako,
ili kutenda haki, na kupenda rehema,
Na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”
Mika 6:8
Wabaptist wanasadiki kuwa Wakristo wanao wajibu wa kufanya yote mawili kwa kueneza injili na kuiishi injili kwenye maisha yao yote. Muinjilist wa Baptist Billy Graham ameandika, “ Sisi kama Wakristo tunayo majukumu mawili, moja, kueneza injili ya Yesu Kristo kama ndio jibu pekee ya mahitaji yake ya ndani. Pili, kuishi maisha ya Ukristo kwenye mazingira yote ya jamii tunayoishi.
Kuishi maisha ya Kikrosto kwenye jamii inayotuzunguka kunahitaji yote mawili huduma na kushiriki masuala la kijamii. Hayo yote mawili kuna uhusiano japo kuna tofauti kati yake. Huduma hujishughulisha na jitihada za kuganga mioyo ya watu waliomizwa – kiroho, kimwili, kiakili na kimawazo. Kujishughulisha katika jamii ni pamoja na kubadilisha mazingira magumu ambayo yanasababisha maumivu. Huduma inalenga kusahihisha makosa. Kushughulika na jamii ni kuzuia mambo kutotokea. Kwa mfano, kuwapa watu chakula ambao wanakosa chakula ni huduma. Kufanya kazi kwa nia ya kuondoa kinachosababisha njaa ni aina ya kujishughulisha kijamii.
Msingi wa Kuishi kwa Injili
Jitihada za Wabaptist kuonyesha ukweli kwenye makosa kumejengwa juu ya imani na mafundisho ya Kibaptistaptist kama vile ukuu wa Kristo na mamlaka ya Biblia.
Kutambua ukuu wa Kristo kunaleta jitihada za kuwa na jamii bora kwa njia ya upendo na haki. Yesu ni Bwana wa wote (Yohana 1:3; Wafilipi 2:9-11). Alisema sio tu kukiri kwamba Yesu ni Bwana (Yohana 13:13) lakini kutenda sawa na vile yeye alivyotenda na ukuu wake (Luka 6:46). Bwana muumba wa kila kitu anatamani kuona kufanya yale anayotufundisha na kufuata mfano wake (Mathayo 7:21-27).
Yesu alifundisha kwamba Amri Kuu ni kumpenda Mungu na wengine. Hii inatoa mwongozo kwa maeneo yote mawili yaani kuishi maisha ya Kikristo lakini pia kuenenda kama vile injili isemavyo kwenye maisha yetu yote (Mathayo 22:36-40). Yesu alionyesha huduma yake kwenye kila hali ya maisha aliyokuwa akiisha (Luka 4:18-19). Mafundisho ya Yesu yanatuonyesha namna alivyokuwa akishughulia changamoto za jamii, kama vile za kifamilia na kiserikali (Mathayo 19:3-12; 22:15-22). Yesu alitoa mfano kwa kujitoa dhabihu na kuamuru wanafunzi wake kubeba msalaba na kumfuata. (Mathayo 16:24).
Biblia imeweka baina kila mtazamo wa Kimungu kwenye kila eneo la maisha ya mwanadamu….kwa mtu binafsi, familia, Makanisani, uchumi na utawala wa kiserikali……na ametoa wito kwa watu kufuata huo utaratibu.
Agano la Kale imeandika kusudi la Mungu kwa ajili ya taais na jamii. Manabii walikemea ulafi na vitendo vya uvunjivu wa haki kwa sababu vilikuwa vinapingana na kusudi la Mungu. Manabii waliweka baina namna Mungu alivyokuwa akichukia na hivyo vitendo kwenye jamii iliyokithiri maovu., kuonewa kwa watu masikini, kufanya vita vya hujuma, na uonevu kwa watu wadhaifu. Walitoa wito wa kuondoka na hivyo vitendo vibaya na kutenda haki (Yeremia 5:25-29; Hosea 6:6; Amosi 5:21-24; Mika 6:6-8). Walionyesha mfano wa “unabii wa muumini” na ukuhani wa muumini.”
Agano Jipya imeandika kwamba Wakristo wa Makanisa ya kwanza walionyesha msisitizo wa kusudi la Mungu kwa haki, kibinadamu, kikawaida na kijamii pia. Kwenye ulimwengu ambao viongozi wa serikali waliokithiri kwa rushwa, viongozi wa Kanisa wanafanya jitihada za kuelimisha mwenendo wa Mungu ili hawa viongozi wa serikali wawe raia mwema (Warumi 13:1-7). Kipindi ambacho watu wengi, kama wanawake na watumwa, walichukuliwa kama wadhaifu, Viongozi wa Kanisa walisisitiza usawa kwa watu wote katika Kristo (Wagalatia 3:28). Hali zinazojitokeza katika jamii ili kujali wenye mali na kudharau masikini kulikemewa vikali na viongozi wa Kanisa (Yakobo 2:1-9).
Hatua za kuishi Ipasavyo Kiinjili
Wabaptist wana hatua mbalimbali ili kuhakikisha kuisha namna ya injili isemavyo kwenye maisha yote. Baadhi ya hizo zipo ili kuimarisha msingi wa taasis za mfumo wa jamii, kama vile familia, biashara na serikali. Wengine hufanya vibaya kwenye jamii, kama vile, kutotoa haki, rushwa na tabia mbaya.
Mbaptisti mmoja mmoja kuimarisha jamii yenye mwenendo mzuri kwa kuishi sawa na mafundisho ya Biblia kila siku ya maisha yake……. Kwenye familia, eneo la kazi, masuala ya siasa, Kanisa na maeneo ya burudani….. na kuonyesha jitihada za kukemea kuenea kwa matendo mabaya kwenye hayo maeneo.
Makanisa ya Baptist, Makanisa kwenye majimbo na Kanda aptist churches, associations of churches and conventions kupitia vipindi mbalimbali vinavyoandaliwa kwa kuonyesha jitihada za kuwa na ubinadamu katika jamii kwenye usawa.
Wabaptist husadiki uinjilisti wa matendo pamoja na kushuhudia kutaleta matokeo mazuri kwenye kuibadilisha jamii. Matendo ya kijamii peke yake sio uinjilisti, na uinjilisti peke yake sio matendo ya kijamii. Hata hivyo, uinjilisti kwa njia ya mazungumzo kunaweza kusaidia watu kujenga mazoea ya kubadilisha hali za watu wengine. Uinjilisti wa kweli pamoja na ufuasi thabiti huleta mabadiliko makubwa kwenye maisha, na wale wanaobadilika huleta mabadiliko kwa ulimwengu mzima.
Wabaptist, huhubiri, kufundisha na uwandishi ili kuendeleza mtazamo wa Biblia juu ya kuwa na jamii bora, ili kukabiliana na matendo maovu, na kuhamasisha watu na mashirika kujihusisha ili kuleta matendo mema kwenye jamii. Wahubiri wa Baptist wamesadiki mafundisho ya Kibiblia juu ya kuleta hali ya mabadiliko duniani. Waandishi wa Kibaptist wamekuwa wakiandika makala nyingi sana zenye kuelezea umuhimu kuishi maisha ya utaua
Wabaptist wamekuwa wakiandamana na maonyesho mbele ya umati wa watu ili kuleta mabadiliko kwenye jamii .
Hujihusisha hata na masuala ya siasa hata pia kuwahamisha watu kupiga kushiriki kwenye chaguzi.
Hufanya mazungumzo na viongozi wa serikali ili kuja na hatua madhubuti za namna ya kuthibiti masuala mbalimbali yanaleta madhara kwenye jamii, kama ile ukame, picha za aibu, umasikini, njaa na ubaguzi wa rangi.
Hujiunga na madhehebu mengine ili kuunda mashirika ili kushughulikia masuala maalum yanayosumbua kwenye jamii, kama vile unyanyasaji wa watoto, kukataa maisha ya ubadhilifu, ulevi na machafuko ya kuingilia uhuru wa dini.
Wakati mwingine, Wabaptisti wamejiingiza kwenye , vita vya silaha ili kuleta jamii yenye amani na usawa, mfano wakati wa mabadiliko ya Marekani.
Kwa kawaida, Jitihada za Kibaptist zimekuwa za amani , kama vile vitendo vya uonevu kwenye maeneo ya kazi wakati wa vita juu ya uhuru wa kuabudu na kampeni kwa haki.
Changamoto za kuiishi kwa injili
Jitihada za kuitumia injili ili kuleta usawa mbele ya jamii kumekutana na changamoto mbalimbali. Wakati watu, Makanisa na taasis za Baptist husisitiza kufuata maagizo ya Yesu kwamba sisi ni chumvi na nuru (Mathayo 5:13-14), mara nyingi hukumbana na kukataliwa na kunyanyaswa.
Kuiishi injili mara nyingi huleta mashaka. Kuiishi injili ni vigumu pia kwa sababu mara nyingi kunatokea hali ya kutokubaliana linapokuja suala la masuala yapi hupaswa kushughulikia kwanza. Kutokukubaliana kwingine kunaweza kujitokeza kwa sababu ya hatua gani ambazo zinaweza kutumika ili kutatua tatizo husika.
Watu wengine huuliza swali la uhalali wa jitihada za kufanya ili kuondoa changamoto ndani ya jamii. Hayo mashaka yanaweza kusababisha kushindwa kuiishi namna ya injili kwenye maisha yetu.
Hali ya kutojali na hali ya kutofautiana nalo huleta kipingamizi kwenye kutekeleza hili jambo la kuiish injili. Kwa batai mbaya, watu wengi huchagua kuacha haya masuala kwa wengine ili kushughulikia haki na uwazi ulimwenguni..
Wabaptist hujitahidi kukabiliana na hizi changamoto kwa njia mbalimbali. Huhimiza watu kutafuta uongozi na nguvu za Roho Mtakatifu juu ya changamoto zipi ambazo kwenye jamii zinaleta shida na njia gani zitumike ili kuzishughulikia. Huhimiza Makanisa kufundiza mafundisho ya Biblia yanayoelezea namna ya kuiishi maisha ya utaua. Huunda mashirika ya dhehebu ili kukabiliana na changamoto za kijamii. Hushirikiana na watu mbalimbali kutoka kwenye madhehebu mengine ili kuondoa maovu kwenye jamii.
Hitimisho
Wabaptist kwa kila mmoja wao, Makanisa na mashirika mengine hujitahidi kuiishi injili ya Bwana wetu Yesu Kristo katika maisha yao. Wabaptist wako vizuri kwenye uinjilisti na huduma, lakini pia wanajihusisha kwenye maeneo maalum ili kuleta ubinadamu sawa kwenye jamiia. Hutoa gharama kwa kufanya hivyo kwa sababu huamini kuwa dunia inaweza kuwa mahala salama pa kuishi, kwa sababu wanaamini ni mafundisho ya Kristo, na kwa sababu ya uasili wa Kristo ndani yao kufanya hivyo (Wagalatia 2:20).
“Kiukweli sisi kama raia wa Kikristo hatuna mamlaka na kukubaliana na mambo yanayoendelea
Kwenye jamii hadi pale makusudi ya Kristo yatakapo kamilika kwa watu wote.”
Billy Graham