Wabaptisti huamini Kanisa Kujitegemea

“Mimi ni Alfa na Omega,I am the Alpha and the Omega,
wa kwanza na wa mwisho; ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwenye haya Makanisa saba yaliyoko Asia.”
Ufunuo 1:11

Ni nini maana ya  kujitegemea kwa Kanisa?  Neno la kujiendesha lilitokana na lugha ya kigiriki lenye maana ya kujitegemea. Kwamba, Kanisa linao uwezo wa kujiendesha lenyewe bila msaada kutoka nje wa kibinadamu wa wowote ule. Kiukweli linajiendesha lenyewe, kwa sababu Kanisa kila wakati linapaswa kutambua mamlaka na uweza wa Yesu kama Bwana.

Kujitegemea kwa Makanisa ya Kibaptisti

Kila Kanisa la Kibaptisti linajitegemea. Kuwa kanisa linalojitegemea ni nafasi kubwa ya kulifanya liwe Kanisa la Kibaptisti. Wabaptisti hutumia neno “Kanisa” ikiwa na maana ya Kanisa la mahali lenye waumini waliobatizwa na sio kama dhehebu la Baptist. Hivyo basi, kwa kutumia neno “Kanisa la Wabaptisti” sio sawa endapo una maana ya dhehebu la Kibaptisti. Kila Kanisa la mahali linajitegemea, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa Kanisa la Baptist.

Kujitegemea huku kuna maana ya kwamba, kila Kanisa la mahali la Baptist, pamoja na mengine, humtafuta Mchungaji wanaomtaka, huamua aina ya ibada ambayo inapaswa kufanywa, hujiamuria masuala ya fedha na kuelekeza kwenye masuala ya makanisa mengine bila kuingiliwa wala kusimamiwa.  Muundo wa uendeshaji wa dhehebu la Baptist kama vile ushirika wa makanisa ya eneo fulani, kwa maana ya jimbo, kanda au taifa hayana mamlaka ya Kanisa la mahali la Baptist. Kwa kila umoja au muunganiko wa umoja huu utajaribu kuingilia masuala ya Kanisa la mahali ni kwenda kinyume na mafundisho ya Wabaptisti na heshima waliyo nayo.

Being autonomous, a Baptist church recognizes no governmental control over faith and religious practice. Although Baptist churches obey the laws of governments related to certain matters, they refuse to recognize the authority of governments in matters of doctrine, polity and ministry (Matthew 22:21). Baptists have consistently rejected the efforts of any secular government entity to dictate to a church what to believe, how to worship or who should or should not be members. Such refusal to bow to the demands of governments has cost Baptists dearly.

Wabaptisti pia wamekataa mtindo wa baadhi ya madhehebu ambayo mamlaka kutoka kwenye viongozi wa dhehebu husika ndiyo hutumika kwa kipi cha kuamini na kuabudu. Wabaptisti wamesisitiza kwamba hakuna mwanadamu mwenye mamlaka juu ya Kanisa la Baptist. Ni Yesu tu ambaye ni Bwana wa Kanisa.

Athari kwa Kanisa la Baptist kujitegemea kule Marekani inasadikika zinatoka ndani ya dhehebu la Baptist kuliko kutoka kwenye mamlaka ya nchi au kutoka kwenye makundi mengine ya dini. Kwa wakati mwingine ushirika au umoja wa Wabaptisti na Jumuiya zao huona kama viongozi husika wanayo mamlaka juu ya Makanisa.

Hili linaweza kutoaka na uelewa mdogo juu ya huu mfumo wa kimamlaka kwa Makanisa. Majimbo na Jumuiya ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya dhehebu la Baptist na huchangia sana jitihada za Wabaptisti kuwafunza wanafunzi waliokomaa na wafuasi waliokomaa katika Yesu Kristo kwa kuwahudumia watu kwa jina lake. Hata hivyo, hawana mamlaka juu ya Kanisa la mahali. Kila Kanisa la mahali linao uchaguzi wa kushiriki kwenye huo umoja au hapana kutokana na matakwa ya ushirika husika..

Uwepo wa hali ya kujitegemea ndani ya Baptist, imesababisha matokeo ya uelewa hafifu, mashtaka, na hata mateso. Serikali mbalimbali zimewashitaki Wabaptisti kama wasaliti, na baadhi ya madhehebu wamewachukulia kama wazushi. Kuna aina mbalimbali za jinsi ya kuliongoza Kanisa zikitajwa, na aina ya uongozi wa ushirikishwaji hufanywa na kundi chache la madhehebu ya Kikristo. Kwa nini haswa Wabaptisti wanasisitiza kujitegemea kwa Makanisa?

Msingi wa Kibiblia juu ya Kujitegemea kwa Kanisa

Suala la Kanisa kujitegemea kwa Wabaptisti halijawekwa kama kitu cha ziada kwenye mafundisho ya Kibaptisti. Ni jambo ambalo ni la msingi kwenye mafundisho ya Kibaptisti. Hakuna aina ya uongozi ambao huongeza radha kwenye mafundisho ya Kibaptisti na desturi zao.

Biblia ndiyo yenye mamlaka juu ya imani na mwenendo wa Wabaptisti, Wabaptisti huamini kwamba Biblia hukubaliana na suala la Kanisa kujitegemea. Wakati wa Agano Jipya, kila ushirika wa Kanisa la mahali uliweza kujitegema. Kila moja lilikuwa linajitegemea chini ya mamlaka ya Yesu Kristo. Walikuwa wakishirikiana kwa njia ya ushirika, lakini hakuna mwanadamu au kundi lolote kuweza kuingilia mamlaka ya ushirika husika.

Kwenye Agano Jipya kwenye sura ya pili na tatu ya Kitabu cha Ufunuo huonyesha kwamba kila Kanisa kati ya Makanisa saba huko Asia ndogo ambako ufunuo ulikusudia lilikuwa ni la kipekee, chombo tofauti na hayakuwa chini ya uongozi wa aina yeyote zaidi ya Yesu Kristo. Yesu Kristo aliyefufuka na kuinuliwa alipewa mamlaka kwa Makanisa.

Makanisa ya Agano Jipya kwa wakati wao walichaguliwa miongoni mwao waumini kwa ajili ya kusaidia waumini wenye mahitaji mbalimbali (Matendo 6:3-6), walikubaliana ni watu wa aina gani kwa ajili ya kutoa huduma fulani (Matendo 13:1-3). Hatua hizo zote zilichukuliwa kwa msaada na uongozi wa Roho Mtakatifu  bila mwiingilio kutoka nje, au kutoka kwa viongozi wa kiroho, kama vile Mtume Paulo, walitegemea ushawishi na mifano kuliko kuamriwa wakati wa kuandika Agano Jipya.

Zaidi ya hapo, wakati wa Wakristo wa Agano Jipya hawakukubaliana na jitihada za serikali na viongozi wa dini mbalimbali na desturi zao (Matendo 4:18-20; 5:29). Wakristo wa kwanza walisisitiza juu ya kujitegemea kutoka kwa pande zote viongozi wa dunia na wa dini.

Imani zingine za Kibaptisti na hali ya Kujitegemea kwa Kanisa

Kujitegemea kwa Kanisa ni jambo ambalo msingi wake ni kutoka kwenye Biblia ikiwa ni msingi wa mafundisho ya Kibaptisti. Kwa mfano, ukuu wa Kristo, imani yenye thamani sana kwa Wabaptist, inayohusiana na hali ya kujitegemea. Kristo ni Bwana wa kila mmoja na kila kanisa. Yesu, na sio mtu fulani wala kikundi fulani, ndiyo mwenye mamlaka. Ukuu wake juu ya Kanisa hujidhihirisha ndani ya kanisa kupitia washirika wa Kanisa, watu waliomwamini na kumfuata kama Bwana. (Waefeso 4:1-6).

Watu waliokoka kwa hiari yao hukutana kwenye makundi na kuanzisha Kanisa. Biblia imeeleza wazi wazi kwamba ni wale tu waliozaliwa mara ya pili ndio wanapaswa kuwa washirika wa Kanisa (Matendo 2:47). Hawa watu wameokolewa kwa imani na kupitia zawadi ya neema yake Mungu ya wokovu ndani ya Kristo, hivyo wote ni watakatifu kwenye mzani moja (Warumi 5:1-2; Waefeso 2:8-9). Hivyo basi, hakuna awaye yote wala kikundi chochote ndani au nje ya Kanisa kuwa na “mamlaka juu ya” awaye yote au Kanisa (1 Petro 5:3)

Mungu ameweka utashi kwa kila mmoja kuwa na uhuru wa kumjua na kufuata kusudi la Mungu. zaidi ya hapo, kila mmoja anayemwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi huwa kuhani muumini (1 Petro 2:9) akiwa na uweza ya kumfikia Mungu moja kwa moja. Hakuna  mpatanishi mwingine, kama vile kuhani wa kibinadamu, anayehitajika (Waebrania 9:11-14; 10:21). Kila kuhani muumini analo jukumu ya kutumia vema wajibu wake wakutumia vema huu ukuhani. Sehemu moja wapi ni kuwa na mahusiano mazuri baina ya moja na mwingine katika yali ya upendo wa Kanisa kwenye ushirika na kuhusika kwenye utawala wa ushirika husika wa Kanisa, ikiwa ni kutimiza kusudi la Bwana kupitia kusoma Neno, Maombi na Uongozi wa Roho Mtakatifu.

Kama vile washirika wote wa Kanisa wanavyopaswa kuwa na sauti sawa kwenye ushirika wa Kanisa lao, ndivyo ilivyo kwa kila ushirika kiroho kuwa sawa na wengine. Hakuna Kanisa, au utawala wa Kanisa, uko juu zaidi ya Kanisa lingine. Hakuna mwenye mamlaka juu ya mwenzake. Kwa maana nyingine, kila Kanisa linapaswa kujitegemea.

Utawala wa ushirika wa Kanisa na suala la kujitegemea kwa Makanisa ni mambo ambayo huenda sambamba. Kimoja hakiwezi kuwepo kila kingine. Kama watu binafsi au kundi ndani ya ushirika wa Kanisa ndio wenye mamlaka ndani ya Kanisa, hapo maana yake hakuna hali ya kujitegemea, na hakuna utawala shirikishi wa Kanisa.

Hitimisho

Japo changamoto zipo juu ya Kanisa kujitegemea, msingi wake ni mafundisho ya Biblia kitu ambacho ni cha muhimu sana kwa utambulisho Wabaptist hivyo kunapaswa kutunzwa na kuimarishwa. Sehemu inayofuata tutazungumzia hizo changamoto.

“Kila Kanisa daima ni huru na linajitegemea, juu ya kila mamlaka ambayo imewekwa na watu wa ulimwenguni, kila Kanisa ni nyumba ya Kristo.”
Muswada wa haki sawa,  Sehemu. 1
wa Umoja wa Majimbo ya Baptist, October 8, 1840