Utawala wa Kanisa

“Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.”
Warumi 12:5

Ni nani anatawala Kanisa lako? Ni nani alikupa uongozi wa Kichungaji? Ni nani anaamua mgawanyo wa fungu la kumi na sadaka na matumizi yake? Ni nani anaamua ni mafundisho yepi ya kufundisha na desturi za kufuata? Ni nani mwenye mali za Kanisa? Mfumo wa Kanisa na utawala hutoa majibu ya haya maswali.

Ni nini maana ya Utawala wa Kanisa?

Mfuno ni jinsi taasis, mfano kama Kanisa, huendesha shughuli zake- hizi taratibu zitaongoza namna mambo kama utawala, maamuzi, muundo na uongozi. Wabaptist hutofautiana na madhehebu mengine ya Kikristo kwenye suala la muundo. Huu utofauti na kwa sababu ya ushirika wa Wakristo unavyotawala.

Sababu moja kubwa kati ya Wabaptisti na madhehebu mengine hakuna mtu au kikundi chochote nje ya Uhsirika Wabaptisti anayo mamlaka juu ya Kanisa licha ya mafundisho ya imani na taratibu za kuabudu. Zaidi ya hayo, washariki wote ndani ya ushirika wa Kanisa wana haki sawa juu ya uongozi wa Kanisa.

Baptist church governance often is termed “democratic.” In a sense it is. In a democracy, all of the people have equal voices in decision making. No individual or group of persons is in control. Such is to be the case in a Baptist church. One way that democratic governance is practiced is that each member of the church has the right to vote on matters at church business meetings.

Kwa wengi ambao sio Wabaptisti, na hata kwa baadhi ya Wabaptisti hili ni jambo geni la jinsi ya utendaji kazi wa Kanisa. Kutoa mamlaka ya kuliongoza Kanisa kwa mtu ambaye hana mafunzo maalum, elimu au wito linaonekana ni jambo la kijinga. Kwa nini Wabaptisti wanathubutu kuwa na aina hii ya mtindo?

Ni nini msingi wa Uongozi wa Ushirika?

Kwa Wabaptisti mafundisho sio sehemu tu ya mfumo wao bali pia ndio msingi wa mfumo wa utawala. Hivyo basi, msingi wa mafundisho ya Wabaptisti vinahusiana na uongozi wa ushirika.

Ukuu wa Yesu Kristo.  Unajieleza wazi wazi, Wabaptisti hawaamini kwenye utawala wa Kanisa kwa njia ya Kidemokrasia “Kidemokrasia” ni neno la kisiasa lenye maana ya “kutawala watu”. Kwa Wabaptisti mamlaka ya mwisho ya Kanisa hayamo kwa watu lakini kwa Yesu Kristo. Yesu ndiyo Kichwa au Bwana wa Kanisa (Waefeso 4:15; Wafilipi 2:11). Pengine tafsiri nzuri ya kuelezea utawala wa Kanisa ndani ya Baptist ni “Demokrasia ya Kimungu” kukiwa na maana utawala wa Mungu kwa watu wake.

Mamlaka ya Kibiblia. Wabaptisti huamini kuwa utawala wa ushirika ni mfano wa namna Kanisa la Agano Jipya lilikuwa likifanya. Kwa mfano, washariki, washiriki wa Makanisa ambao walikuwa kwenye huduma mbalimbali,  hakuwa mtu mmoja wala kundi fulani, walifanya maamuzi makubwa (Matendo 6:1-6; 13:1-3; 15:22; 2 Wakorintho 8:1-13).

Wokovu ni kwa Neema tu kwa njia ya Imani. Wabaptisti wanaamini kuwa watu wote ambao walikolewa walikuja kwa neema ili kutumika kwa imani katika Kristo, sio kwa matenda mema, au hadhi ya utu, au kitu kingine chochote (Waefeso 2:8-10). Chini ya msalaba hali ni sawa. Kwa hiyo, hakuna Mbaptisti ambaye ni bwana wa mwingine. Hivyo, Kanisa linapaswa kuongozwa na watu wote chini ya mamlaka ya Kristo.

Uweza wa Roho na Ukuhani wa Muumini. Watu wanao uweza wa Kimungu kumjua na kufuata Kusudi la Mungu. wale waliitikia kwa njia ya imani zawadi hii ya neema kutoka kwa Mungu ya wokovu anafanyika kuwa “muumini kuhani” (1 Petro 2:9; Ufunuo 5:1-10). Kila muumini ana uwezawa kuzungumza na Mungu moja kwa moja kwa njia ya kusoma Maandiko na maombi na yuko huru kwa msaada wa Roho Mtakatifu kutambua kusudi la Mungu. zaidi ya hayo, kila muumini ni sehemu ya “ukuhani wa kifalme” ambapo Yesu Kristo ndiyo Kuhani Mkuu (Waebrania 7 – 10). Huu ukuhani ni ushirika ambao kila muumini kuhani anapaswa kutafuta mwongozi wa Kimungu kama sehemu ya umoja ya huo ushirika.

Kuzaliwa Upya kwa Ushirika wa Kanisa kwa Aliyebatizwa.  Wabaptisti wanaendelea kusisitiza juu ya mafundisho ya Biblia kwamba Kanisa ni wale wote waliokolewa kwa kumwamini Kristo pamoja na kushiriki kwenye ubatizo wa maji mengi. Kanisa, kwa hiyo, ni ushirika wa waumini waliobatizwa, au tunaweza kusema, ni jamii ya makuhani wa waumini. Uongozi wa Kanisa hauko kwenye mikono ya mtu mmoja au baadhi  yao bali ni kwa washirika wote.

Maswali na Changamoto zake

Dhana ya uongozi wa ushirika ni wa Kibiblia na lina uhusiano wa mambo ya msingi ya mafundisho ya Kibaptisti. Hata hivyo, watu wakati mwingine wanakuwa na maswali juu ya muundo:

Ni nani Mwenye Mamlaka?  Kwenye dhana ya kitudia, Rais au Mkurugenzi Mkuu wa taasis hudhaniwa kama ndiye mwenye mamlaka. Hivyo, ni hali ya kawaida kwa watu kudhani hata Kanisa lina huo mfumo wa uendeshaji. Hata hivyo, kulingana na Biblia na pia mafundisho makuu ya Wabaptisti, Wabaptisti husisitiza kwamba Kristo ndiye “mwenye mamlaka” ya Kanisa na washarika wanapaswa kutafuta na kufuata kusudi la Kristo kwa Kanisa lake.

Sio Mchungaji mwenye mamlaka Kikanisa? Wazee Je?  Biblia huonyesha kwamba Wachungaji wana jukumu kubwa la kufanya ndani ya Kanisa (1 Timotheo 3:1-7).  Hata hivyo, majukumu haya sio yale yenye mamlaka bali yenye kutumikiana kama watumwa, uongozi wa kiroho, “sio kuwa chini ya wale walioaminiwa” sio kuwa juu ya wale waliokuamini” (1 Petro 5:2-3). Biblia kuonyesha kwamba Wachungaji wana majukumu makubwa, na washarika wanapaswa kuwaheshimu majukumu ya hawa watumishi na kuonyesha kuwa kwa njia hiyo “kazi yao ni ya furaha, na sio mateso “(Waebrania 13:17). Biblia pia imeelezea sifa za wazee wa Kanisa (1 Timotheo 3:8-13), lakini wazee wanapaswa kuwa watumishi na sio viongozi wa Kanisa.

Ni kwa namna gani maamuzi hutolewa?  Kwa sababu ni watu wanaojiendesha, Makanisa ya Kibaptisti hutofautiana kwenye baadhi ya maeneo namna ya kufanya maamuzi.  Mfumo wa Baptist unatoa wito kwa kila muumini kuwa huru kwenye kufanya maamuzi sawa na kusudi la Kristo kwa Kanisa lake. Hata hivyo, sio kwa vitendo kwamba kila muumini anahusika kwenye maamuzi. Hata hivyo, makanisa yanafuata hatua mbalimbali namna ya kuendesha shughuli za Kanisa. Makanisa mengi yameweka hii mwongozo kwa njia ya kuwa na katiba na kanuni pia.

Kwa asilimia kubwa ya makanisa, ushirika hutoa mamlaka kwa kamati ya Kanisa, kwa Mchungaji/au kwa viongozi wengine wenye wajibu wa kufanya maamuzi. Hawa huleta maamzui ya mambo makubwa kwa ajili ya ushirika kuidhinisha. Mara nyingi maamuzi ya kamati, Mchingaji/ au viongozi wengine hupitiwa kwanza na baraza la wazee kwa ajili ya kuidhinisha kabla kuleta mbele ya Kanisa kwenye kikao cha Kanisa nzima.

Ni dhahiri, washirika wote wanapaswa kushiriki kikao cha Kanisa nzima. Kwenye makanisa mengi, vikao vya Kanisa hufanywa kabla ya ibada na vinafanyika mara kwa mara, kama labda kila baada ya robo mwaka. Vikao maalum vinafanyika na kamati kwa njia ya kupiga kura mfano kama wanahitaji mchungaji mwingine.

Uongozi wa namna huu hauna upungufu? Unaweza ukawa na upungufu kwa njia mbalimbali, lakini ni nzuri kwa sababu hujumuisha washarika wote kwenye maamuzi juu ya mwenendo na huduma ya Kanisa. Kwa sababu ya mfumo huo Kanisa linaimalika, watu hujisikia kuwa ni sehemu ya Kanisa kuliko walivyo upande mwingine. Kanisa kuwa kwenye mikono ya watu kumeonyesha mafanikio makubwa katika kutimiza kusudi la Kanisa, kama vile uinjilisti, ufuasi na huduma.

Hitimisho

Huu mtazamo wa namna ya kuliongoza Kanisa ni dhahiri na ngumu kuutekeleza. Kwenye somo litakalofuata tutajifunza baadhi ya hizo chngamoto. Wabaptisti huamini kwamba licha ya ugumu, wanapaswa kufuata huu mfumo wa uongozi kwa sababu wanafuata mfano wa uongozi wa Kanisa la Agano Jipya na ni vizuri kuendelea kufuata msingi wa mafundisho ya Kibiblia ambayo Wabaptisti kufuata.

“Kila mfumo usio kuwa na demokrasia
kuna mahali hufifisha Ukuu wa Kristo.”
E. Y. Mullins
Mihimila ya Dini