Wabaptisti: Ukuhani wa Muumini au Waumini?
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingine katika nuru yake ya ajabu.”
I Petro 2:9
“Kila muumini ni kuhani, yaani kote mbele za Mungu na kwa kuwasaidia waumini wenzake na hata watu wengine ulimwenguni ambao Kristo alikufa kwa ajili yao.”
Kutoka Sisi Wabaptisti , James Leo Garrett Jr. (mhariri mkuu)
Kusema kwamba Mbatisti ni kuhani ni jambo la ajabu sana kwa watu wengine. Lakini sisi ni makuhani. Kila mmoja wetu, kiukweli Wabaptisti wanasisitiza kwamba kila mmoja aliyemwamini Yesu kama Bwana ni kuhani, yaani kuhani wa waumini. Dhana ya ukuhani ni ya msingi sana kwa Mbaptisti. Kama yalivyo mafundisho mengine kwa Baptist, tunafafanuzi mbalimbali juu yah ii dhana, lakini sote tuna thamini ukweli wa kibiblia juu ya ukuhani wa waumini.
Ni nini maana ya kuwa Kuhani?
Kuwa kuhani kunahusisha fursa na uwajibikaji. Kwenye Agano la Kale, kuhani alikuwa na sehemu maalum kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Makuhani walikuwa na wajibu maalum kwenye kuabudu, kama vile kuteketeza sadaka. Walikuwa kama wapatanishi kati ya Watu na Mungu.
Kuhani Mkuu, kiongozi mkuu, ni yeye tu, ambaye aliweza kuingia Patakatifu pa Patakatifu kwenye hekalu ya Wayahudi. Hili eneo maalum na muhimu lilitengenashwa na maeneo mengine ya hekalu lakini pia kutenganishwa na makuhani wengine na waabudu kwa pazia kubwa.
Kwa kupitia maisha, kifo na ufufuo wa Yesu, kila kitu kilibadilika. Hakukuwa na umuhimu wa kuteketeza wanyama, kwa sababu Kristo, Mwana Kondoo wa Mungu, alijitoa mwenyewe kama sadaka ya dhambi ya kuteketezwa. Hili lilifanyika mara moja tu na halitajirudia kamwe.
Wakati Yesu anasulubiwa msalabani, pazia kubwa la hekalu “lilichanika katikati kutoka juu hadi chini”(Mathayo 27:51), kuonyesha kwamba Yesu, Kuhani Mkuu, amefanyika kuwa patanishi kati ya Mungu na Mwanadamu. Hakuna haja tena ya aina ya makuhani wa Agano la Kale kuwepo. Ni kweli, wale wote waliomwamini Yesu wamefanyika kuwa makuhani na wanauwezo wa kumfikia Mungu moja kwa moja. Wanadamu kama wapatanishi hawahitajiki tena. Tunaweza kwenda moja kwa moja kwa Mungu kwa njia ya maombi, kutubu, kusifu na kuabudu. Bahati iliyoje!!
Kuwa kuhani kuna wajibu wa kutimiza. Kwenye Agano la Kale, kuhani kwa kawaida alikuwa anamwakilisha Mungu kwa watu.. leo hii, kuhani muumini ana wajibu wa kuwashirikisha watu wengine juu ya Mungu, kwa namna zote mbili maneno na kwa matendo.
Kuhani muumini ana wajibu wa kushuhudia upendo wa Mungu kama alivyoonyesha Yesu Kristo na kuonyesha upendo wa Mungu kwa kuwatumikia watu kwa jina lake. Huu wajibu hufanya kwa njia mbalimbali kwa Wabaptisti, kama vile uinjilisti, umisheni, huduma na matendo ya jamii ili wengine waweze kuona faida.
Ni wapi dhana ya Ukuhani wa Waumini ilipotokea?
Martin Luther, kiongozi kwenye Mapigano ya Mabadiliko, mara nyingi amehusishwa ha hii dhana ya ukuhani wa waumini. Luther alipingana kabisa na Kanisa la Waroma juu msisitizo wao kuwa hili lilikuwa jukumu maalum la Makuhani wa Kanisa la Roma.
Luther alisisitiza kuwa kila muumini ni kuhani, mwenye uwezo wa kumfikia Mungu moja kwa moja.Hakuwa na maana ya kuodoa majukumu ya Wachungaji lakini alionyesha kuwa watu wote, sio tu wachungaji, wana jukumu la kikuhani. Na hata kabla ya Luther kulisema hilo kwenye mfumo wa Kanisa la Ulaya, makundi mbalimbali ya Kikristo yalisisitiza ukuhani wa waumini.
Lakini, dhana ya ukuhani wa waumini kwa Wabaptisti haikutokana na mafundisho ya Luther wala kutoka kwenye kikundi chochote cha Kikristo, bali kutoka kwenye Agano Jipya. Kwa kuzingatia maandiko mbalimbali kwenye Agano Jipya, Wabaptisti wamekuwa wakisisitiza kwamba kila mtu anayemwamini Bwana Yesu Kristo anao uweza wa kumfikia Mungu moja kwa moja. Kila mmoja anawajibika moja kwa moja kwa Mungu. Kila mmoja anao uweza wa kushirikisha upendo wa Mungu.
Ukuhani wa Muumini
Ukuhani wa kila muumini wa Baptist hudhani huenda sawa na dhana nyingine, ya uweza wa roho. Kila mmoja anao uwezo kutoka kwa Mungu kujua na kufuata kusudi la Mungu. Uamuzi wa kumfuata Kristo kama Bwana na Mwokozi ni uamuzi binafsi; hakuna awezaye kuufanya kwa niaba ya mwingine. Kitendo cha kuwa kuhani muumini ni zawadi kutoka kwa Mungu, sio kwa jitihada za mwanadamu, unakuja na wokovu.
Kila kuhani muumini anawajibika kwa matendo yake. Kila muumini anao uweza wa kwenda moja kwa moja kwa Mungu bila kupitia kwa mwingine. Kila mmoja anao uweza wa kusoma na kuitafsiri Biblia bila shinikizo kutoka kwa viongozi wa dini kwa kuwaongoza nini cha kuamini.
Makuhani wa waumini wote wako sawa mbele za Kristo (Wagalatia 3:26-28). Yuko kuhani mkuu mmoja tu, naye ni Yesu Kristo (Waebrania 7:23 – 8:13).
Kila muumini kuhani anao wajibu wa kujitoa kwa ajili ya Kristo na kuwashuhudia wengine Kristo kwa maneno na matendo. Kama Petro alivyosema: “mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Petro 2:9 ).
Kwa hiyo, Kanisa halina kuhani mmoja tu. Kwa kawaida anao wengi ambao huonyesha upendo na msamaha wa Mungu na kuonea hururma na kusaidia moja na mwingine
Ukuhani wa Waumini
Agano Jipya pia husema juu ya ukuhani wa waumini. Waumini makuhani ni sehemu ya mwili wa Kristo. Wanajenga jamii ya waumini. Japo kila kuhani muumini anawajibika kwa Mungu, waumini makuhani wote ni ndugu kama ndugu katika Kristo.
Hiki kipengele cha jamii ya muumini kuhani kuonyesha kwamba ukiwa Mkristo kuna maana ya kuwa na shirika na watu wwaumini wengine. Huu ushirika upo ili kuweza kutiana moyo na kumsaidia kukua katika Ukristo na huduma pia. Ni jinsi gani inaweza ikawa huzuni ukaishi maisha ya kujitenga na waumini wenzako.
Ushirika wa makuhani waumini pia husaidia kuitafsiri Biblia na kulielewa kusudi la Mungu. Ni kweli kila muumini kuhani anao uweza wa kusoma na kuitafsiri Biblia akiwa mwenyewe, waumini waelevu na wenye utashi zaidi watapenda kujifunza zaidi na kupata uelewa zaidi kutoka kwa waumini makuhani wengine. Kwa kutafuta mafundisho ya waumini makuhani wa zamani na kwa kutafuta hekima na maarifa kwa wale wa sasa, watu husaidika katika kuielewa Biblia na kusudi la Mungu.
Mfumo wa Kanisa la Baptist limejikita kwenye dhana ya ukuhani wa waumini. Kanisa ni mkusanyiko wa watu ambao wametumia utashi wao waliopewa na Mungu kwa kumwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi kwa hiari na kuwa na shirika na waumini wengine.
Kila muumini kuhani kwenye ushirika wako sawa. Kwa hiyo, hakuna mwenye mamlaka juu ya yote. Kwa hiyo maamuzi hufanya na jamii ya makuhani wakitazamia kujua zaidi kusudi la Yule ambaye ni kichwa cha Kanisa, Kuhani Mkuu, Yesu Kristo. Hufanya haya kwa njia ya maombi, kujifunza Biblia, kuitafakari Biblia, kujadili na kufanya maamuzi kwa pamoja.
Hitimisho
Kwa hiyo, hiki ni nini? Ukuhani wa muumini au ukuhani wa waumini? Sio kati ya hili/au ni yote/na.
Maana ya “ukuhani wa muumini” huwasilisha mkazo wa Biblia juu ya mtu mmoja na uweza wa roho. Maana ya “Ukuhani wa muumini” huwasilisha mkazo wa Biblia umuhimu wa jamii na ushirika.
Kulingana na historia kwenye hali zote za maisha, hofu imekuwa ikitanda juu mtu mmoja na kikundi cha watu. Wabaptisti hawajakwepa hii hofu. Tunafanya vema tunapokataa kumwinua mmoja kuwa juu ya watu wengine, bali kuwafanya watu wote kuwa sawa.