Uhuru Wabaptisti: Changamoto na Faida
“Kwa kuwa walipo wawili watatu,
wamekusanyika kwa jina langu,
name nipo papo hapo katikati yao.”
Mathayo 18:20
Upeo wa mawazo potofu, maswali mbalimbali, vitisho na changamoto mbalimbali zimetawala kwenye desturi za Baptist. Licha ya hivyo faida zake ni kubwa kuliko changamoto zinazohusiana na uhuru.
Makanisa ya Baptist hujitegemea chini ya ukuu wa Kristo. Hakuna mtu awaye yeyote au kikundi chochote ndani ya Baptist mwenye mamlaka ya kuamrisha ni kipi cha kufuata.
Baadhi ya Mawazo Potofu ju ya Uhuru wa Baptist
Dhehebu la Baptist limeundwa na ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ushirika wa Kanisa la mahali, umoja wa Makanisa (Kijimbo), Kanda na Jumuiya za Kitaifa na makundi mengine mbalimbali. Kwa mujibu wa desturi za Kibaptisti, haya makundi yote yana uhuru.
Hata hivyo, mahusiano ya huu uhuru wakati mwingine unaeleweka vibaya. Kwa mfano, wengine hudhania ni kwa “ngazi” Fulani kwenye Kanisa la Baptisti, kwa mfano, kama vile ngazi ya Kanisa la mahali, ngazi ya majimbo, ngazi ya Kanda na ngazi ya Taifa. Mawazo ni kwamba ngazi za juu zina mamlaka kwa ngazi za chini. Hii sio sawa kwa desturi ya Kibaptisti.
Ngazi ya Kitaifa haipangi mambo ya ngazi ya Kanda nini cha kufanya, na ngazi ya Kanda haipangi mambo ya ngazi ya jimbo nini cha kufanya. Kwa sababu hiyo, kila ngazi ni huru, ndani ya muundo wa Baptisti. Zaidi ya hapo, hakuna ngazi yeyote kati ya hizo ambayo inayo mamlaka juu yaw engine. Hatua zinazochukuliwa na uongozi wa kitaifa wa Baptist, hazina mamlaka juu ya makundi ya Baptist yaliyopo na majimbo yake na hata Makanisa.
Sambamba na hilo, Kanisa la mahali halina mamlaka juu ya jimbo au kanda. Zaidi ya hapo, majimbo na ngazi zingine za kijumuiya, kwa kuwa ni huru, wanayo mamlaka ya kufanya maamuzi na kumkubali nani atakuwa au atakaa kama kiongozi na pia kuamua ni taasis gani ndani ya Baptisti ambazo wanaweza kushirikiana nazo au la.
Masuala mengine yanayohusu Uhuru wa Baptist
Hata kama hii dhana ya uhuru wa Baptist umeeleweka vema, namna ya kuutumia huu uhuru ndani ya Baptist kwa nyakati zote bado haujawekwa vizuri.
Wakati muundo wa Baptist kimsingi ulipangwa kuwa ni mkusanyiko wa makundi madogo madogo ya ushirika wa waumini waliobatizwa, suala la uhuru lilikuwa ndogo sana kuliishi. Kama umoja wa Wabaptisti, taasis, Kanda na taifa na mashirika mbalimbali zimetokana na maisha ya Baptist, suala la uhuru halikuwa jambo rahisii kama walivyokuwa awali.
Kwa mfano, maswali mengi yamekuwepo kuhusiana na suala la uhuru kwenye taasis za Kibaptist. Kwa mfano, vyuo vikuu, taasis za afya na vituo vya kulelea watu wazima na watoto wasio na uwezo. Kwa mfano, maswali hujitokeza kwenye suala la namna ya kuziendesha taasis za Kibaptisti. Kwa mfano, vyuo vikuu, vituo vya malezi mbalimbali, taasis za afya. Kama wote au baadhi ya wadhamini wa taasis hizi huchaguliwa na chombo kingine cha Kibaptisti, kama vile ngazi ya kanda au kitaifa, ni uhuru gani hizi taasis unao
Masuala mengine ya uhuru unahusisha ushirika wa kanisa la mahali. Mengine ni pamoja na namna ya kuanzisha makanisa mapya. Kwa mfano, Mmoja akaomba wito kutoka kwa jimbo, kanda, taifa au Kanisa la mahali ili kutoa msaada kwa ushirika mpya. Kwa kawaida upatikanaji wa Mchungaji hauko mkononi mwa ule ushirika mpya lakini pia hujumuisha na wale waliotoa msaada wa kuanzisha. Hili sio kwamba ni kukiuka hali yan uhuru ndani ya Kanisa kwa sababu ule ushirika unakuwa bado hujasimikwa kama Kanisa.
Athari ambazo zinaweza kujitokeza kwenye hii dhana ya Uhuru Wabaptisti
Athari juu ya hali ya kujiamuria mambo ndani ya Baptist zipo hata leo hii. Zinatoka pande zote mbili nje ya Baptist na hata ndani ya Baptist yenyewe.
Changamoto zitokanazo na nje ya ushirika zinajitokeza endapo baadhi ya mashirika kutaka kuanza kuwa na mamlaka juu ya Kanisa kwamba ni kipi cha kuamini/ au ni jinsi gani ya kuendesha huduma. Serikali za kidunia wakati mwingine husababisha msukumo fulani. Wabaptisti wamekuwa wakiendelea kukataa, na kushikilia imani ya kuwa na dini huru na kwamba masuala ya Kanisa yasiingiliwe na serikali.
Mashirika ya Kibaptisti nje ya Kanisa yanaweza kuleta huo msukumo pia na kusababisha Mfano mwingine wakati mwingine nguvu kutoka ngazi ya jimbi, kanda au hata taifa inaweza kutumika kuamulisha Kanisa kufuata maamuzi yao juu ya kufuata mafundisho fulani na kusema endapo hawatafanya hivyo basi watajitoa kusaidia kwa namna yeyote ikiwepo pamoja na kifedha.
Japo hatua hizo zinaweza kudhoofisha uhuru wa Kanisa la mahali, linapaswa kukumbuka pia kwamba kila shirika/taasis ya Kibaptisti nazo pia zina uhuru wa kufanya maamuzi na zina haki pia ya kuamua ni Makanisa yapi ya kufanya nao shirika. Zaidi ya hapo, Kanisa la mahali sio kwamba lianze kupiga magoti kwao bali linapaswa kuona lipi la kufuata ambalo ndani yake ni kutimiza kusudi la Kristo kwa Kanisa. Kwa mfano jimbo linaweza kusema “hapana” kwa kile ambacho Kanisa linataka, na Kanisa pia linaweza kusema “hapana” kwa kile ambacho jimbo linataka.
Athari za kujiamuria mambo ndani ya Kanisa zinaweza kujitokeza endapo washirika hawajishughulishi na kanuni za Kibiblia na hivyo kutoa nafasi kutoka kwenye mashinikizo nje ya Kanisa. Washirika wa kanisa wanapaswa kujali, kuondoa ujinga na hofu ambavyo vinaweza kupelekea wao kuacha kufurahia, dhana ya Kibiblia juu ya uhuru.
Changamoto zingine juu ya Uhuru wa Baptist kujiamuria
Masuala mengine yanapaswa kuweka bayana kwa nia ya kuufanya huu mfumo wa kuwa Kanisa huru kutenda vema. Kwa mafano, dhehebu nzima halina mamlaka juu ya Kanisa linalosumbua. Kama Kanisa linaleta aibu, dhehebu halina mamlaka ya kuingilia kati na kuleta mabadiliko na hata kuondoa jina la “Baptist”. Kama Kanisa lina mgogoro wa ndani kwa ndani, hakuna chombo cha dhehebu ambacho kinaweza kuingilia kati na kuweka mambo sawa. Kama Kanisa lina uhaba wa fedha, hakuna njia ya kulifanya dhehebu kufika na kutatua tatizo hilo. Hata kama Kanisa limeomba msaada kutoka kwa taasis za dhehebu la Baptist, halitoi uhuru wake.
Suala lingine linalohusu Wachungaji na wengine ambao wameajiriwa na Makanisa na taasis mbalimbali za Baptist. Dhehebu kwa ujumla halina mamlaka ya kuwaadibisha au kuwatetea watu wa jinsi hiyo kwa sababu ni waajiri wa taasis huru ya Kibaptisti na sio dhehebu.
Changamoto inayohusiana na kutimiza wajibu wa Kibiblia juu ya umisheni, elimu ya Kikristo na ukarimu. Kwa kufika mbali zaidi, suala la kujitegemea limepelekea kujitenga kitu ambacho kumelifanya Kanisa kushindwa kutimiza ndoto zake vizuri juu ya umesheni na huduma zingine.
Kama huu uhuru tafsiri yake ni kwamba kila mmoja au Makanisa yako huru kufanya kile ambacho kwao ni sahihi, matokeo yake ni hasi. Wakati wowote ule ikumbukwe kuwa ukuu wa Kristo kiwe kipaumbele. Watu binafsi na Makanisa wako huru kufanya kikubwa linapendezwa mbele ya Kristo.
Wabaptisti hawajakaa kimya wamejaribu kutatua hizi changamoto juu ya dhana ya kujitegemea na kuwa huru kwa njia ya kushiriki kwa hiari, Ni somo ambalo litakalofuata baada ya hili kwenye haya mafundisho.
Faida za kuwa Kanisa huru la Kibaptisti
Kama changamoto zipo kwa sababu ya uhuru, kwa nini kuziacha ziendelee? Sababu ya msingi ni kwamba suala la uhuru linatokana na ukweli wa Kibiblia. Kama hakuna sababu nyingine nje ya hiyo, basi Wabaptisti wanapaswa kushikilia huo msimamo wa uhuru wa Makanisa.
Uhuru pia unasaidia Wabaptisti kwenda sawa na masuala mengine ya msingi kama vile uongozi shirikishi wa ushirika, ukuhani kwa waumini wote na uweza wa roho.
Kwa nyongeza, uhuru hutoa nafasi kwa Kanisa moja la mahali ni namna gani bora linaweza kuwafikia na kufanya huduma kwenye jamii lililopo. Uhuru unachochea uwepesi na ubunifu zaidi.addition
Uhuru wa Kanisa unasisitiza ukweli kwamba ndani ya Kanisa la Kibaptisti kila muumini ana wajibika kwa Kanisa lake. Huo mtazamo wa uwajibikaji unaweza ukawa na faida kwamba kila muumini analitambua vema kanisa na kufanya sehemu yao kwa ajili ya afya ya Kanisa wakati wa kutimiza huduma mbalimbali.
Zaidi ha hayo, uhuru unasaidi kutoa nafasi ya utetezi linapotokea suala la mashtaka. Dhehebu halina wajibui kwa maamuzi yatakayotolewa na ushirika wa mahali, na ushirika wa mahali hauna wajibu juu ya maamuzi ya kanisa lingine au ngazi zingine ndani ya dhehebu la Baptist.
Hitimisho
Uhuru wa Baptist umetunzwa muda mrefu tangia karne zilizopita kwa gharama kubwa sana. Hiki kizazi kinahitaji kufanya jitihada pia za kuutunza ili kizazi kijacho nacho kiweze kufuata.
“Kwa Wabaptisti wengi, uhuru yamekuwa machafuko.
Huu ni ukweli pale ambapo labda Kanisa au kila Mbaptisti anasema, “Naweza kufanya lile ambalo nitapendezwa nalo!” Wote wanapaswa kufanya lile ambalo litampendeza Kristo na kutimiza kusudi lake.”
Herschel H. Hobbs
Imani ya Wabaptisti na Ujumbe wake